Skip to content

Barua pepe au ujumbe wa moja kwa moja huondoa unyanyasaji mtandaoni katika mijadala ya hadharani kwani kuna mashahidi hali inayofanya macho yote ya watu yawe kwako na watu wanaweza kuchukulia vitu katika mtazamo tofauti.

Unapokumbana na barua pepe au ujumbe wa moja kwa moja unaouona kuwa wa matusi, anza kwa kujiuliza ikiwa ujumbe huo unakufanya ukose amani. Fuata hisia zako. Ikiwa huna uhakika, rafiki au mwanafamilia wanaweza kukusaidia kufanyia kazi baadhi ya maswali ili kufanya tathmini ya tishio. Ikiwa unaamini kuwa wewe au wapendwa wako mko katika hatari, tafuta mahali ambapo unahisi kuwa salama zaidi kimwili, mjulishe mwajiri wako na uwasiliane na vyombo vya sheria vilivyo katika eneo lako. Iwapo hujisikii salama kumuhusisha mwajiri wako au na wasimamizi wa sheria, waarifu marafiki na washirika unaowaamini na ufikirie kuripoti kwa mashirika ya ndani, ya kitaifa, au ya kimataifa yanayounga mkono uhuru wa vyombo vya habari na mashirika ya haki za binadamu kama vile International Association of Women in Radio and Television, Kenyan chapter (IAWRT). Hakikisha unaainisha vitisho vyote.

Ikiwa umepokea barua pepe za matusi au ujumbe wa moja kwa moja, lakini hakuna kidokezo kinachoonesha kuwa wewe au wapendwa wako mko hatarini, Kuna baadhi ya hatua unazoweza kuchukua:

 • Piga picha ya “skrini”, weka kwenye kumbukumbu na/au toa nakala ya ujumbe iwapo vitisho hivyo vitajirudia siku zijazo. Utahitaji rekodi ya jumbe zote endapo yataendelea kujitokeza na kukufanya uhusishe vyombo vya dola. Hakikisha kuwa unafuata hatua za mwongozo huu wa hatua za kurekodi manyanyaso uliyopokea.
 • Ripoti barua pepe au ujumbe wa matusi kwa mtu anayeendesha jukwaa. Ikiwa ujumbe unatoka kwenye Gmail, Twitter, Facebook, n.k. unapaswa kuwa na uwezo wa kuripoti kwa wahusika wenyewe.
 • Usisambaze barua pepe. Iwapo unahitaji kuwatumia wengine, nakili ujumbe kama ilivyo na uwatumie. Kusambaza barua pepe kunaweza kusababisha upoteze data muhimu ya mwelekeo uliopo katika barua pepe ya mwanzo ambayo inaweza kuhitajiwa na vyombo vya dola hapo baadaye.
 • Tumia kipengele cha “zuia mtumaji” katika huduma yako ya barua pepe. Huenda hili lisikomeshe kabisa barua pepe za matusi, kwani mtumaji anaweza kuunda barua pepe mpya kila wakati ambapo atakutumia ujumbe, lakini ni mahali pa kuanzia na utapumzika kwa muda.
 • Weka Chujio katika huduma yako ya barua pepe. Iwapo ungependa kuwa chonjo dhidi ya mtu anayekunyanyasa mtandaoni na/au umepanga kumuweka rafiki yako akusaidie kufuatilia jumbe za matusi, fikiria pia kuunda kichujio cha barua pepe ambacho kitapeleka barua pepe za matusi kwenye akaunti hewa. Kwa njia hii si lazima uone matusi hayo mara kwa mara, lakini ikiwa wewe au mshiriki wako unayemwamini mnahitaji kuangalia hali ya barua pepe ambazo mnyanyasaji anaendelea kukutumia, utakuwa na mahali pa kuzihifadhi.
  1. Chuja huduma kwenye Gmail
  2. Chuja huduma kwenye Yahoo
  3. Chuja huduma kwenye Outlook
  4. Chuja huduma kwenye Apple
 • Fikiria kumjulisha mwajiri wako, hasa ikiwa ujumbe unahusu vitisho, matamshi ya chuki, unyanyasaji wa kingono, picha za ngono zisizo na ridhaa, au unyanyasaji wowote unaokufanya ukose amani, kutishia usalama wako. Mwajiri wako anaweza kutoa msaada zaidi na anaweza kuhitaji kufuatilia matukio ya unyanyasaji katika taasisi nzima. Ikiwa huna uhakika jinsi ya kuwasiliana na mwajiri, Mwongozo wa Kuzungumza na Waajiri na Mawasiliano ya Kikazi unaweza kukusaidia.
 • Mjibu mtumaji endapo tu utahitajika kujibu. Labda kama una uhakika kwamba maudhui ya ujumbe hayana vitisho vya moja kwa moja lakini ni bora kama hutojihusisha na mtumaji kabisa.

Majibizano kama hayo huwa hayana tija na mara nyingi yanaweza kusababisha manyanyaso zaidi. Iwapo, ikiwa maudhui ya ujumbe hayatishi na unahisi yatakusaidia kumshughulikia anayekushambulia kwa kumjibu, tafadhali fuata muongozo huu wa namna ya kumjibu anayekushambulia mtandaoni.