Skip to content

Mshirika
Yule anayehusishwa na mwingine kama msaidizi, mtu au kikundi ambacho kinatoa msaada na usaidizi.

Shahidi
Mtu ambaye anaona kitu (kama vile uhalifu) unapotokea.

Kuingilia kati
Ni kitendo cha kuingilia kati jambo, matokeo au chanzo, cha hali fulani au mchakato ili kuzuia madhara yasiweze kutokea.

Mtazamaji
Mtu ambaye yupo mahali husika lakini hashiriki wala kujihusisha katika hali au tukio linaloendelea mahali hapo.

Kama upo hapa, Kuna uwezekano ni kwa sababu umeshuhudia chuki au unyanyasaji kupitia mtandao na hauna uhakika ni kipi cha kufanya kuhusu hilo. Kuna watu wengi wa aina yako:  Wanahabari saba kati ya 10 wa kike nchini Kenya wamepitia unyanyasaji mitandaoni wakitimiza majukumu yao.

Pale unaposhuhudia mtu mwingine akilengwa kwa chuki au unyanyasaji kupitia mtandao, inaweza kukukatisha tamaa kuingilia kati. Itakuwaje kama hajui pa kuanzia au hakuna mtu mwingine wa kuingilia kati? Itakuwaje kama utafanya unyanyasaji ushamiri pasipo wewe kukusudia? Itakuwaje kama wewe mwenyewe ukageuka na kuwa mlengwa wa huo unyanyasaji? Itakuwaje kama unyanyasaji ulio ushuhudia ukakutia kiwewe kwa namna fulani, kufanya iwe ngumu kwako kubakia kwenye jukwaa husika ambapo unyanyasaji huo umetokea?

Haya ni maswali muhimu na ya lazima kujiuliza mwenyewe wakati wa kuzingatia kama ni ndio au la, na ni vipi, utamsaidia mtu ambaye ni mlengwa wa unyanyasaji wa mtandaoni. Lakini ikiwa unahisi unalazimika kumsaidia, na una imani unaweza kufanya hivyo pasipo hatari yoyote kwako, Mtazamaji anapoingilia kati ni moja ya zana yenye nguvu tunayopaswa kuizungumzia katika kupinga chuki na unyanyasaji katika mtandao na kukataa desturi ya kutokujali kuongezeka katika majukwaa ya mtandaoni.

1. Upatie usalama wako kipaumbele

Una kila njia za kuchukua tahadhari kabla ya kutafakari kuhusu suluhisho la unyanyasaji wa mtandaoni. Jiandae wewe mwenyewe mapema, Ili uwe tayari kuwa mshirika. Chukua muda kuimarisha usalama wa mtandao wako kuulinda na kutumika kwa taarifa zako binafsi na wadukuzi. Kama una wasiwasi kuwa kuingilia kati kwenye unyanyasaji wa mtu mwingine kupitia mtandao kutakuweka katika hatari, angalia miongozo ya kutathimini matishio na amini hisia zako. Kumbuka: Kuna njia nyingi za kuwa mshirika mzuri bila kujihusisha moja Kwa moja. (Tazama hapa chini).

2. Tambua aina ya unyanyasaji unaofanyika.

Kufahamu nini hasa ambacho unashuhudia inaweza kukusaidia wewe kufikiria jinsi ya kufanya.

Ni utambulisho wa mshambuliaji wa Facebook ndio unatakiwa kukemewa? Ni uteuzi wa maoni kwenye blog yako uipendayo ikizidi kuwachukiza wanawake, na uko tayari kujaribu kuelekeza mazungumzo upya? Kuna mtu taarifa zake binafsi zimetumika vibaya na wadukuzi na anahitaji msaada kutathmini matishio yao au kutafuta sehemu salama ya kukaa? Kuna mtu kwenye Twitter anatoa matishio ya kufanya vurugu na wewe unahisi Kuna haja ya kuwatahadharisha polisi katika mamlaka ya mtumiaji? Tambua ni aina gani ya unyanyasaji unaofanyika na angalia kuhusu unyanyasaji katika mtandao Ili ufahamu mbinu mbalimbali.

3. Wasiliana na mlengwa (kama inawezekana).

Kabla hujaingilia kati unyanyasaji wa mtandaoni iwe moja kwa moja au kwa njia ya kuutumia umma, fikiria uhusiano wako na mlengwa na tanguliza mahitaji na kipi kinawapa mashaka. Njia yenye ufanisi zaidi ni kuwatafuta na kuwauliza ni msaada gani watauthamini hasa kama unakusudia kupata kusikilizwa na umma kwenye jambo hilo au kuhusisha utumikaji wa sheria.

Kama mtu ambaye ni mlengwa wa unyanyasaji yupo tayari kuungana na wewe, anza Kwa kumsikiliza na kumuuliza ni jinsi gani utamsaidia. Baadhi ya watu wanaweza kuwa wamezidiwa na hawana mawazo ya ni kwa namna gani utaweza kuwasaidia na kwenye jambo gani unaweza kuwapa chaguo au kwa kuwasikiliza na kuwahurumia. Wengine wanaweza kuwa hawataki msaada wowote, labda ni kwasababu wanataka hali itoweke kimyakimya, kwenye jambo hilo matakwa yao yanatakiwa yaheshimiwe. Jaribu kutomwambia mlengwa ni vipi anatakiwa kujisikia au kufanya.

Hannah Schacter, mtafiti wa udaktari katika Chuo Cha Southern California’s, Idara ya Saikolojia, anasema jamii inapoonesha hali ya kuguswa na kutoa msaada kwa muathirika inaweza kuwa na nguvu kwasababu Wana uwezo wa kubadilisha kanuni na kuhamasisha watazamaji wengine wa mtandaoni kushiriki kwenye jambo hilo. Lakini kwa kuwa na ufahamu wa faida na vikwazo vya Umma kuingilia kati inaweza kusaidia kutofautisha kati ya ufanisi na uwezekano wa madhara ya mikakati. Walengwa wanaojisikia kuwa wametengwa na jamii, ameelezea kuwa wanaweza kupata ugumu zaidi kuomba msaada, na inaweza kuwa muhimu kuwapa usaidizi ambao hawajaomba. Kwa upande mwingine, baadhi ya walengwa wanaweza kupendelea kushughulikia unyanyasaji wenyewe na /au kuhisi msaada wa Umma utadhoofisha uwezo wao binafsi wa kukabiliana nalo. Ndio maana kuwasiliana na mlengwa kama inawezekana daima ni njia bora zaidi.

Kumbuka: kama umeshindwa kuwasiliana na mtu aliyenyanyaswa, Kuna vitu bado unaweza kufanya kutoa msaada, kama vile kupaza sauti zao au kuripoti unyanyasaji dhidi yao kwenye majukwaa husika ( tazama zaidi hapa chini). 

4. Tafuta njia sahihi ya kutoa msaada.

Right to Be,” Wanaharakati wa kukomesha unyanyasaji,” wametengeneza mfumo mzuri sana kwa ajili ya watazamaji kuingilia kati, D’s Tano: kuvuruga, mjumbe, nyaraka, chelewa, na njia ya moja kwa moja. Cha kustaajabisha kuhusu D Tano ni kwamba moja tu ndiyo inahusu kujihusisha moja kwa moja, kwa maneno mengine, unaweza kutoa msaada na ushirika kwa namna zote hata kama hujisikii vizuri kujihusisha moja kwa moja.

Kuvuruga

Kama umeamua kuvuruga unaweza “kupunguza matukio kwa kuyatafsiri” (Right to Be). Wanyanyasaji mara nyingi wanajaribu kuwanyamazisha wahanga wao. Unaweza kuwazuia kwa:

  • Kukuza (kupaza) maudhui ya asili yaliyotumwa na mhanga wa shambulio hilo la unyanyasaji.
  • Kuondoa umakini kutoka kwenye unyanyasaji na kwa mnyanyasaji Kwa (Kwa mfano) kujibu kwa kutumia picha ya mtoto wa mbwa au kutumia mfululizo wa hashtag zenye maudhui ya kufurahisha
  • Kuripoti maudhui ya unyanyasaji na akaunti ya mnyanyasaji kwenye mamlaka ya jukwaa ambalo unyanyasaji umefanyika. Ingawa sio kila mara kwa jukwaa kuchukua hatua ila ni mbinu nzuri ukitumia, fuata miongozo ya kuripoti unyanyasaji mitandaoni.

Mjumbe

Kwa kutafuta mjumbe, unaomba “usaidizi, rasilimali, au msaada kutoka kwa mtu mwingine” (Right to Be). Kuna nguvu kwenye idadi, na wanyanyasaji wa mtandaoni wanaweza kuwa na uwezekano mdogo wa kulifuata kundi zima kuliko mtu mmoja. Kama mlengwa ametuma chapisho maalumu la kuomba msaada, wasaidie kwa kusambaza ujumbe kwa mitandao yako. Unaweza kuhamasisha Jumuiya ya mtandao inayounga mkono umma (Kwa machapisho) au binafsi (kama watumiaji wako wa barua pepe, makundi yako ya kitaaluma, kikazi au binafsi). Tuma ujumbe kwa jumuiya hizo ili kuwaonesha wapi ambapo unyanyasaji huo wa kimtandao unafanyika kama vile jina la jukwaa husika, ili kuomba msaada huo. Jumuiya inayokuunga mkono inaweza kukusaidia:

  • Kupaza maudhui ya mtu ambaye amenyanyaswa.
  • Kuteka (kuondoa) umakini kutoka Kwa mnyanyasaji Kwa kutumia vichekesho au maudhui yasiyoendana.
  • Kumripoti mnyanyasaji kwenye majukwaa pale yanapotokea- na hata kuambatanisha majukwaa ili kuongeza umakini zaidi.

Nyaraka

Njia mojawapo nzuri ya kumsaidia mtu aliyefanyiwa unyanyasaji ni kufuatilia maongezi yao (Kwa tishio, chuki,) na nyaraka ni kwa kupiga picha ya skrini (inayoonesha ujumbe wenye maudhui ya unyanyasaji) na kuhifadhi kiunganishi (links) cha taarifa husika.

Angalia kumbukumbu kuhusu unyanyasaji mtandaoni Kwa taarifa zaidi kuhusu kwanini hii ni muhimu sana. Weka akilini, kuangalia picha za skrini za unyanyasaji inaweza kukupa kiwewe Kwa wale wanaopokea mwishoni, kwa hiyo pale unaposhirikisha taarifa ulizozikusanya, kuwa makini kutoa onyo la wazi kuhusu kuwepo kwa maudhui ya kuogofya. Unaweza kujaribu kitu kama. “Kurekodi unyanyasaji ni muhimu sana, lakini nimegundua inaweza pia kukupa kiwewe, kwa  hiyo nimechukua picha za skrini na kuhifadhi mfumo wa taarifa kwa ajili yako kwenye hii folda. Unaweza kulihifadhi sehemu nyingine salama kama utalihitaji tena kama utalihitaji tena baadaye.”

Ucheleweshwaji (mfano, kuwasiliana)

Unyanyasaji wa mtandaoni unaweza kufanya mtu akajitenga (mara nyingi huwa ndio lengo la mnyanyasaji), kwa hiyo kuwasiliana na mtu aliyefanyiwa unyanyasaji huo ni njia nzuri inayoweza kuleta athari chanya. Unaweza:

  • Kumsikiliza na kumpa msaada wa kudhibiti hisia zake. Daima kumsikiliza mhanga bila kumhukumu. Hakikisha unatumia busara na hekima, na zingatia matakwa yao.
  • Thibitisha kuwa kinachowatokea siyo sawa na wala wao si wasababishaji, wakumbushe kuwa hawako peke yao.
  • Sambaza rasilimali- ikiwemo mwongozo huu.
  • Toa msaada maalumu ( “Ninaweza kukusaidia kuripoti, kutunza kumbukumbu au Kuimarisha usalama wa mtandao wako?”)

Kama una uhusiano wa karibu na mhanga na unajua kuwa wanaogopa kuhusu usalama wao au usalama wa wapendwa wao, fikiria kuwapa sehemu salama ya kuishi, Kama vile nyumbani kwako au nyumbani Kwa rafiki yako wa karibu unayemuamini.

Moja Kwa moja

Kujihusisha moja kwa moja umejikita katika utoaji jibu “unyanyasaji kwa kutaja ni nini kinaendelea au kukabiliana na mnyanyasaji.” Hii ni ile wengi wetu tunafikiri pale mtazamaji ataingilia kati- na muda mwingine inaweza kuwa ni ushirikiano wenye athari zaidi – lakini unaweza kuwa na madhara, kwako na kwa mlengwa wa unyanyasaji. Mnyanyasaji anaweza akahamishia unyanyasaji wako kwako au kuongeza unyanyasaji kwa mhanga. Ndio maana ni muhimu kuweka kipaumbele kwenye usalama wako na kuwasiliana na mhanga kila inapowezekana.  Kama unajihisi umejipanga kuingilia kati Moja Kwa moja, hivi ni vitu unavyoweza kuvijaribu:

  • Ingia kwa kuunga mkono, kuthibitisha, au maoni yenye kujenga, ujumbe, au himiza kujibu kwenye maudhui ya mtu ambaye ni mhanga wa unyanyasaji.
  • Chapisha kauli ya mshikamano ambayo inarudisha nyuma lengo na inapinga unyanyasaji wa mtandaoni, kwenye majukwaa ambapo unatokea. Mtaje mnyanyasaji, onyesha kwanini si sawa, na itisha mkutano wa hadhara kuhimiza wengine kuukataa. Kama wewe ni miongoni mwa kikundi au taasisi inayohusishwa na taarifa rasmi ambayo inaeleza wazi kwanini unalaani unyanyasaji wa mtandaoni. Mradi wa Tor unatoa mfano mzuri wa kauli ya mshikamano inayoweza kuitumia Kwa niaba ya mhanga wa unyanyasaji wa mtandaoni.
  • Fichua uigaji na omba msaada kuripoti hilo kwenye majukwaa.
  • Tumia upendeleo au madaraka kuangalia ukweli kwenye madai ya uongo.
  • Tumia ucheshi.

Hizi ni dondoo muhimu za kujifunza mapambano ya kuongea hadharani. Kwa miongozo ya kina angalia miongozo yetu Kwa usalama wakati wa kumkabili mnyanyasaji wako mtandaoni.

  • Unaweza kulaani chuki na unyanyasaji bila kuingiliana na mnyanyasaji. Laani kitendo na siyo mtu, na weka mifano kwa wengine kuwa tabia hiyo haifai na haitakiwi kuvumiliwa.
  • Usijihusishe na unyanyasaji wewe mwenyewe, siyo kwasababu ya kuingilia kati kwa mtazamaji ni kwa ajili ya kuvunja mzunguko wa chuki na vurugu, lakini kwa sababu mnyanyasaji anaweza kukusudia kujaribu kukufanya wewe kama njia ya kufanya madhara.
  • Wahamasishe wengine kuingilia kati na kuandaa mtandao wa usaidizi. Kuna nguvu kubwa inayotokana na watu.

5. Pia Jiangalie Mwenyewe

Kushuhidia tabia za unyanyasaji mtandaoni, vitisho vyenye madhara, kauli za chuki, na michoro ya picha inaweza kusababisha madhara hata kwa washirika wakubwa. Usione aibu kama ukipitia hisia za uchovu na kuzidiwa- unatakiwa kujiangalia mwenyewe ikiwa unataka kuendelea kuwa mshirika mzuri kwa wengine katika majukwaa ya mtandaoni. Tembelea kipengele cha ustawi na jamii ndani ya mwongozo huu Kwa taarifa zaidi kuhusu jinsi ya kujiangalia mwenyewe ikiwa unapitia unyanyasaji mtandaoni.

Ili kuelewa mambo yanayoathiri uwezekano wa mtazamaji kuingilia kati. Nick Brody, Profesa wa masomo ya Mawasiliano katika Chuo Cha Puget Sound, amefanya utafiti kwa mtazamaji anayeingilia kati na kugundua viashiria vitatu vyenye umuhimu kwenye kuamua kama ni sawa au la Kwa mtazamaji kuchukua hatua ya kuingilia kati unyanyasaji: idadi ya watazamaji, kutojulikana pamoja na Ukaribu na Mhanga. Watazamaji wengi na watazamaji wakubwa zaidi wasiojulikana wote wanauhusiano na uwezekano mdogo wa kuingilia kati, wakati uhusiano wa karibu kati ya mtazamaji na muathirika mara nyingi unaashiria uwezo mkubwa wa kuingilia kati.  Kuwa na uelewa wa jambo hilo kunaweza kusaidia kuongeza hisia za mtazamaji, na kupelekea kuelewa vizuri jinsi ya kukabiliana na unyanyasaji-  Kwa kufahamu au kutofahamu. 

6. Kuwa mwaminifu kwako mwenyewe

Fanya tathmini ya uaminifu ya ukosefu wa haki kwako binafsi. Weka akilini kuwa watu ambao wanakuwa walengwa wanaweza kuwa na historia ya kufanyiwa udhalimu ambayo wewe binafsi hujaipitia. Kufanya tathmini ya uaminifu Kwa ukosefu wa haki kwako binafsi, ukosefu wake, sehemu muhimu ya kuwa msaidizi – siyo mwokozi.  Angalia mwongozo huu wa Melissa Harris- Perry’s juu ya kuwa mshirika mzuri kwenye kutetea haki za wanawake Kwa dondoo zaidi.

Kumbuka: ulimwengu wa mtandaoni ni ulimwengu halisi. Usijaribu kuushusha uzoefu wa mtu katika mtandao Kwa kufikiria kinachotokea kwao kwenye mtandao hakitakuwa na maana zaidi kuliko kitakachotokea kwao nje ya mtandao. Kinachotokea mtandaoni kina matokeo halisi kwenye kazi zetu, mahusiano yetu binafsi, afya ya akili, na uzalishaji mali na pia yanaweza kupitia kwenye maisha yetu nje ya mtandao, na kinyume pia. kulingana na Nick Brody, ulimwengu wa mtandaoni unaweza kuzidisha madhara ya unyanyasaji na uonevu kwa kuwa na uwezekano wa uadui wa mtandaoni. Tukio pekee katika ulimwengu usioonekana, Brody anasema, unaweza kuonekana na mamilioni ya watu na hivyo basi inaweza kuwa na madhara makubwa Kwa muathirika katika afya ya akili na pia maisha yao binafsi.