Sehemu za maoni na uwanja wa ujumbe zinajenga jukwaa la kujihusisha katika mijadala na mikutano ya watu wenye akili na uelewa unaoendana. Lakini pia inawasaidia kutojiingiza katika mashambulizi yanayokimbia hoja na kumlenga mtu binafsi au kusumbuliwa na wababe wanaopenda kuibua migogoro.
Vifuatavyo ni vidokezo vitakavyokuandaa na namna ya kushughulika na unyanyasaji mtandaoni kwenye majukwaa haya
- Hakikisha utambulisho wako hauoneshi taarifa binafsi. Hii inajumuisha jina lako, umri, dini, jinsia au kitu chochote kinachohusiana na wewe. Baadhi ya watu wanajivunia utambulisho wao na kutaka kila mmoja afahamu yeye ni nani mtandaoni, lakini wengine wanaweza kuwa na shaka kwamba taarifa hizi zinaweza kutumiwa dhidi yao na watu wanaofanya unyanyasaji mtandaoni. Ni wewe tu unaweza amua ni utambulisho gani ni salama kuutumia katika mitandao ya kijamii.
- Iwapo utahitajika kuweka anwani ya barua pepe wazi katika mijadala ya mtandaoni, hakikisha kuwa umetumia barua pepe ambayo haijaunganishwa na maisha yako ya binafsi au ya kikazi na haioneshi taarifa binafsi.
- Fahamu sera za usimamizi za mijadala. Baadhi ya mijadala huwa na msimamizi ambaye hutekeleza sheria za maadili; wengine hawana. Ukichagua kushiriki katika mijadala ya mtandaoni isiyodhibitiwa, fahamu kuwa lugha ya matusi, picha, vitisho vya vurugu, n.k zinaweza zisiondolewe mara moja—au kabisa—hata kama zinakiuka masharti ya matumizi ya jukwaa.
- Tambua taratibu za malalamiko katika jukwaa. Kwa njia hii, endapo utashambuliwa moja kwa moja kwa njia inayokiuka sheria na masharti, utajua ni nani hasa wa kumtumia ujumbe ili kuripoti malalamiko yako.
- Jitoe na Uendelee na Maisha Yako. Mara nyingi, kujibizana na manyanyaso ya mtandaoni kutachochea tu moto wao na kukufanya uwe katika hatari ya kuendelea kushambuliana hata nje ya mijadala. Ukijikuta katika hali hii, ni bora zaidi kujitoa na kutojihusisha na mnyanyasaji. Lakini ikiwa ni jukwaa ambalo ni muhimu kwako, na hutaki kuacha mazungumzo, kuna vitu unaweza kufanya:
Toa kauli nzito moja tu — ukitumia lugha thabiti lakini isiyo ya kichochezi huku ukifuata mwongozo wa kukabiliana kwa usalama na mnyanyasaji wa mtandaoni. Lengo la kauli kama hiyo ni kutumia sauti yako mwenyewe kubainisha kwa nini maudhui ya mshambuliaji ni hatari au si sahihi, lakini inapaswa kueleza bayana kwamba hutotaka kujihusisha katika majadiliano yasiyo na tija.
Orodhesha wadau wanaokuunga mkono kwenye mijadala. Tafiti zinaonesha kwamba, katika baadhi ya matukio, wanyanyasaji wa mitandaoni wanaweza koma na kuacha pindi wanapokabiliwa na shinikizo la jamii likiwataka kuacha tabia hiyo. Iwapo jukwaa lenyewe linachukua muda mrefu kushughulika na mnyanyasaji anayekiuka sheria, jaribu kutuma ujumbe kwenye mijadala ambayo itawataka wengine kuchukua hatua dhidi ya tabia hiyo ya unyanyasaji. Weka ujumbe wako rahisi na unaoeleweka, yaani, “Tuyaweke mazungumzo haya kwa heshima. Onesha kuwa huvumilii maneno ya kikabila hapa kwa kuchapisha #Endonlinegenderbasedviolence sambamba na ujumbe wako unaofuata.” Mnyanyasaji hatoweza kumjibu kila mtu anayechapisha machapisho mtandoni yanayohukumu tabia yake. Ingawa jiandae kwani kuna uwezekano kwamba hasira ya mnyanyasaji inaweza kuongezeka pindi watu wengi watakavyo muandama – katika hali hiyo, ni bora ukijitoa na kukaa kimya.